Palitokea mama mmoja alikuw
tajiri sana.
Alikuwa ni mfanyabiashara
mkubwa na alikuwa akimiliki meli nyingi ambazo zilikuwa zikifuata bidhaa nje ya
nchi na kuzileteta ndani.
Siku moja huyo mama aliwatuma
wafanyakazi wake waende wakafate vyakula kwa ajili ya biashara kwani kulikuwa
na uhaba sana wa chakula katika nchi hiyo.
Wafanyakazi walienda na
waliporudi na vyakula yule mama akaviangalia na kuanza kulalamika kwamba
hakuridhika na chakula kilicholetwa hivyo aliamuru wale wafanyakazi wakimwage
kile chakula chote baharini ili wakafate vingine.
Wale wafanyakazi wakamshauri
yule mama kwamba isingekuwa vizuri chakula hicho kumwaga kwani kama hakihitaji
ni vema angewapa watu ambao wanashida ya chakula.
Lakini yule mama hakukubari
ushauri ule cha zaidi alicheka kwa dharau na kuanza kejeli.
Alitoka nje ya meli akasimama
juu kabisa kisha akatoa pete yake ya dhahabu aliyokuwa amevaa kidoleni mwake na
kuanza kusema huku akiwa ameining’iniza ile pete kwenye vidole.
“Nimesema hicho chakula
chote kimwagwe baharini kamwe siwezi kuwa maskini kwa kukimwaga hiki chakula,
kama nitakuwa masikini basi hii pete itarudi tena kwenye kidole changu”, akachukua ile pete akaiachia baharini.
Wale wafanyakazi wakafanya
kama walivyoamuriwa na bosi wao. Wakakimwaga kile chakula wakaenda kufata tena
kingine.
Siku moja akamtuma mfanyakazi
wake akamnunulie samaki mbichi kwani ana hamu ya kula samaki atakayempika yeye
mwenyewe.
Hivyo alitaka akanunuliwe
samaki asiyepasuliwa kwani alikuwa anataku kumtengeneza yeye mwenyewe.
Na kweli aliletewa samaki
kama alivyoagiza. Akamchukua yule samaki akaanza kumpasua, alishtuka sana
alipoona ile pete yake aloitupa kwenye bahari tumboni mwa yule samaki.
Toka siku ile yule mama akawa
masikini wa kutupa, kwani mali zote alizokuwa nazo zilitoweka.
UJUMBE
Siku zote tunaamini kwamba mtoaji kwa kila mtu ni
Mungu. Hivyo kupata kwako wewe leo haimaanishi kwamba hao waliokosa ni kwa
sababu ya uzembe wao.
Kwani kuna wanaopambana na
kutafuta sana tena inawezekana wakawa wanatafuta na kuhangaika kuliko hata wewe
ambaye unajiona kwamba umepata.
Hivyo si vema kutoa kejeli
kwa wasiokuwa navyo na kama unaona unastahili kusaidia, saidia siyo unaweka
NADHIRI.
No comments:
Post a Comment